UVIMBE KWENYE KIZAZI (FIBROIDS)


FIBROID NI NINI?

Fibroid ni uvimbe ambao hutokea kwenye tumbo la kizazi ambao huu uvimbe unaweza kuwa ndani ya kizazi (ukutani mwa kizazi) au ndani ya nyama ya kizazi na nje kwenye ukuta wa kizazi.

Kuna aina kuu zifuatazo za fibroids:

1.Submucosal fibroids(ndani ya kizazi)
2.intramural fibroid(ndani ya nyama za kizazi)
3. Subserosal(nje ya kizazi)
Watu wafuatao wako hatarini kupatwa na ugonjwa huu fibroids
1.Mwanamke ambae hajawahi kupata mtoto mpaka umri mkubwa
2.miaka kuanzia kubarehe mpaka hedhi kukoma
3.kurithi
4.unene
5.kuingia hedhi mapema
Fibroids sio kansa ni uvimbe wa kawaida ambao unakua kwa kutegemea kichocheo cha estrogen hormone ndio maana kuanzia kubarehe mpaka kukoma kwa hedhi ndio wako hatarini. Na mara nyingi uvimbe huu huwaga unaongezeka
kukua sana hasa wakati wa ujauzito kwani vichocheo hivi huongezeka wakati huu kulinda makazi ya mtoto. Ni watu waliofikia kikomo cha hedhi hawapati fibroids.

DALILI ZA FIBROIDS

1.Kutokwa damu kwenye via vya uzazi katikati ya mwezi.
2.kutokwa na uchafu wenye kiaharufu mbaya au ambao hauna harufu lakini mwingi na mweupe.
3.maumivi ya kiuno hasa wakati wa
hedhi ambayo husababishwa na kizazi kujaribu kusukuma huo uvimbe..wengi hupata maumivu makali sana.
4.Tumbo kuuma sana chini ya kitovu.
5.hedhi zisizokuwa na mpangilio
6.maumivu wakati wa tendo la ndoa
7.Kukosa hamu ya tendo la ndoa
8.maumivu makali wakati wa hedhi

Uvimbe unapokua mkubwa unaweza kusababisha dalili zifuatazo.

1.Kukojoa mara kwa mara kwani uvimbe unakandamiza kibofu cha mkojo
2.Mkojo kubaki kwenye kibofu cha
mkojo
3.Haja kuwa ngumu
4.miguu kuvimba
5.kupungukiwa damu

Jinsi fibroids zinavyoweza kuzuia kupata mtoto:

1.Fibriods zikikua sana zinakandamiza mishipa ya kupitisha mayai kutoka kwenye mfiko wa mayai yaani ovari
2.Uvimbe pia unazuia yai lililorutubishwa kujishikiza kwenye kizazi..hasa submucosal fibroids
3.Pia huzuia mfuko wa kizazi kukaza kusukuma mbegu kwenda kwenye mishipa ya kupitisha mayai.

MATIBABU

1.Wanawake wengi wanafibroids ndogo ndogo lakini kwa sababu hazina dalili hahawezi kwenda hospitali na hawa ndo siku wakibeba ujauzito uvimbe unaongezeka kwa sababu ya vichocheo kuongezeka hivyo hawa watu Wanabainika wanapofanyiwa ultrasoudi ndipo wanakutwa navyo.lakini kitaamu.
hospitali hawatibu uvimbe wa namna hii
2.Uvimbe ambao ni mkubwa wenyewe hutibiwa kwa namna zifuatazo (hospital)
A.Dawa ambazo ni gharama sana mfano donazol wengi masikini hawawezi kumdu kununua
B.Vidonge vya maumivu
C.Vidonge vya kuzuia damu kama tranexamic acid na dawa za uzazi wa mpango(COCs)
2.Njia ya pili ni operation nazo zipo operation aina nyingi inategemea na uvimbe ukubwa na wingi wake.
1.Myomectomy hii ni operation ya kuondoa uvimbe mmoja mmoja bila kuondoa kizazi kwa wale wenye uvimbe mmoja uko sehemu nzuri
2.Total abdominal hysterectomy. Hii operation unaondoa kizazi chote kama uvimbe umekaa vibaya na viko vingi.
Hebu jiulize kwa nini mpaka upate
dalili ndo uanze kushughulikia au kutafuta Matibabu ? Kwa nini ubebe ujauzito huku una uvimbe kisa bado mdogo? Au kwa nini ukae na uvimbe kisa bado mdogo?
tambua uvimbe huu sio kansa hvyo
ondoa hofu. Mbali na donazole ambayo ni ya gharama na haishauliwi itumiwe kwa mda mrefu ina sababisha mwanamke anakua na sifa za kiume.
Kuwa na utaratibu wa kufanya uchunguzi wa afya yako.

Comments