*FAHAMU KUHUSU DAWA ZA KUZUIA MIMBA (P2)*

 



Dawa hizi, maarufu kama P2 zimekuwa zikitumika sana kwa wanawake baada ya kuhusika kwenye tendo la kujaamiiana bila kinga kwa lengo la kuzuia na kuepuka mimba.


Hupatikana sokoni pia kwa majina mengine, likiwemo PLAN B. Kiambata hai katika dawa hizi ni homoni ya Levonorgesterol.


Pamoja na kwamba iimekuwa ikitumika sana, bado watumiaji wengi hawafahamu kwa undani kuhusu dawa hii. Yafuatayo ni mambo ya muhimu kufahamu kuhusu dawa hii;

Dawa hii hufanya kazi yake kwa, aidha, kuzuia mbegu ya kiume isifikie yai la kike ili kutunga mimba (kuzuia fertilisation), kupunguza uwezo wa mfuko wa uzazi (uterus) kuhudumia yai lililochavushwa na mbegu ya kiume (kuzuia implantation au kupandikizwa kwa mimba) au kuzuia yai la kike lisitoke katika ovari ili kuchavushwa (kuzuia ovulation).


Dawa hii hutakiwa kutumika tu kama njia ya dharura na sio njia ya uzazi wa mpango, yaani ,isitumike mara kwa mara. Ufanisi wake katika kuzuia mimba ni ndani ya masaa 72 toka tendo la kujamiiana limefanyika. Masaa 24 huaminika kuleta ufanisi wa hadi asilimia 98/99.Inapotumika mapema zaidi ndivo nguvu ya kufanya kazi inakuwa kubwa zaidi.


Matumizi ya dawa hii hayawezi kuondoa ujauzito uliopo tayari au kuzuia magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana kama UKIMWI, kisonono, kaswende, n.k


Dawa hii inapotumika, madhara yake ni kama vile kujiskia vibaya, kichefuchefu na kuhisi kutapika, pia hubadilisha mzunguko wa hedhi na kupelekea hedhi kuja mapema zaidi au kuchelewa. Hedhi inaweza kuwa nzito au nyepesi kuliko kawaida.

Dawa hii inashauriwa na wataalamu wa afya kuwa itumike si zaidi ya mara 3 kwa mwaka kwani baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa matumizi ya mara kwa mara ya dawa hizi yanaweza kupeleka mtu kupata saratani, kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi kutokana na kuvurugika kwa viwango vya homoni (vichocheo) na kuathiri vitu vingine vinavyotegemea vichocheo hivyo.

Kuliko kutumia dawa hizi mara kwa mara ni vizuri kutumia njia zilizo salama zaidi ili kuepuka ujauzito kama kufahamu mzunguko wa hedhi, kutumia kondomu n.k.


like comment and share👍

Comments