Mjumuisho wa tabia za ulaji wa vitu visivyo vyakula huitwa Pica, Hali hii inaweza kumpata mtu yeyote yule,lakini kwa upekee kabisa tujaribu kuona mojawapo ya aina za “Pica” inayotokea kwa wanawake wajawazito ambayo ni ulaji wa udongo. Hali hii hutoa maana ya kuashiria uwepo wa upungufu wa virutubisho muhimu pamoja na uchache wa madini ya chuma mwilini
Hali hii ya kuendelea kula udongo ikikithiri inaweza kusababisha kutokea kwa tatizo la choo kigumu,kuziba kwa utumbo,kuzaliana kwa minyoo kwenye tumbo na utumbo,kuvujia kwa damu tumboni pamoja na maumivu ya tumbo.
Udongo unaweza pia kuzuia ufyozwaji wa madini na virutubisho muhimu mwilini na inaweza pia kusababisha kupotea kwa hamu ya kula. Ikiwa mambo haya yatatokea,mtoto anaweza kukabiliwa na upungufu mkubwa wa virutubisho hivyo nakushindwa kukua vizuri tumboni kwa mama
MUHIMU kwa wanawake wote wajawazito wakijizuia kutumia udongo,pia ni muhimu kwao kufanya uchunguzi ikiwezekana pia kutilia maanani njia mbadala za kujipatia madini ya chuma badala ya kula udongo ili kujiepusha na matatizo yaliyoelezewa hapa. Hali hii (Pica) huweza kujitokeza kwa namna nyingi,wengine ikiwafanya wapende sana kula karatasi,barafu,sabuni,majivu,mkaa,magadi soda pamoja na nguo/matambara
Chukua tahadhari mapema
Comments
Post a Comment