UFARANSA YAPENDEKEZA CHANJO YA ASTRAZENECA KUCHOMWA KWA WALIOTIMIA MIAKA 55 TU

 



Mdhibiti wa masuala ya afya nchini Ufaransa amependekeza kwamba watu ambao wana umri kuanzia miaka 55 pekee ndio wanaopaswa kupatiwa chanjo cha AstraZeneca dhidi ya virusi vya corona. 

Kauli hii iliyotolewa leo inakuja ikiwa ni siku moja baada ya Wakala wa Madawa wa Ulaya, EMA, kuidhinisha matumizi ya chanjo hiyo, ikisema ni salama, licha ya wasiwasi kwamba inasababisha kuganda kwa damu. Nchini Ufaransa, kama ilivyo kwenye baadhi ya mataifa mengine duniani, chanjo hiyo ilikuwa imesitishwa kungojea matokeo ya utafiti zaidi. 

Waziri Mkuu Jean Castex, ambaye mwenyewe ana umri wa miaka 55, alichomwa chanjo hiyo leo hii. Hayo yakijiri, Cameroon imejiunga na mataifa mengine barani Afrika kusitisha matumizi ya AstraZeneca kutokana na wasiwasi huo. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilitangulia kuchukuwa hatua hiyo mwanzoni mwa wiki hii.

#AfyayakoUPDATES

Comments