JUMLA
ya wazazi 35 kutoka kata ya Nalasi wilayani Tunduru wamekatwa baada ya
kukukutwa wakiwafundisha watoto wa kike walio chini ya umri wa miaka 8
mbinu za kuishi na wanaume na kufanya tendo la ngono maarufu kama
msondo.
Mkuu
wa wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya
ulinzi na usalama wa wilaya hiyo alisema, wazazi hao wamekamatwa nyakati
za usiku wakiwa wamejifungia kwenye nyumba mmoja wa waliokamatwa katika
kijiji cha Nalasi wakiwa na watoto hao.
Alisema,
wazazi hao wamekamatwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa msamaria
mwema kwamba,kuna wazazi wamewaficha watoto wa kike wenye umri mdogo na
kuwafundisha mila potofu zinazohusiana na mambo ya ngono ambayo
hayapaswi kufundishwa watoto wadogo.
Mtatiro
alisema, wazazi hao walikamatwa nyakati za usiku wakiwa na watoto hao
wadogo wakiwa katika moja ya nyumba iliyokuwa inatumika kwa shughuli
hiyo.
Pia
alisema,katika msako huo mbali na wazazi hao wamemkamata Kungwi
mmoja,mtendaji wa Rajabu Lusanga na mwenyekiti wa kijiji cha Nalasi Ali
Omari ambao wameshindwa kuchukua hatua dhidi ya wazazi hao licha ya
kuishi jirani na eneo la tukio hilo.
Kwa
mujibu wake shughuli za msondo hazikatwi kufanywa, isipokuwa ni kwa
wasichana wakubwa wenye umri zaidi ya miaka 18 na wale wanatarajia
kuolewa, badala ya kuwafundisha watoto wadogo ambao hawana uwezo wa
kuelewa jambo lolote.
“natoa
wito kwa wazazi wote katika wilaya ya Tunduru tabia ya kuwafundisha
watoto wadogo namna ya kuishi mama na baba jambo hilo tumelipiga
marufuku kwani linachangia sana kuongezeka kwa mimba na wasichana wengi
kuacha shule”alisema, Mtatiro.
Alisema,
vitendo hivyo vinasababisha watoto wadogo wa kike kukosa haki yao ya
kupata elimu na kusisitiza kuwa operesheni hiyo itaendelea katika vijiji
mbalimbali hadi pale jamii itakapo acha kufanya vitendo hivyo.
Baadhi
ya wakazi wa Tunduru wamepongeza jitihada kubwa zinazo fanywa na
Serikali ikiongozwa na Mkuu wa wilaya ya kukomesha baadhi ya mira potofu
ambazo zimekuwa chanzo cha kuongezeka kwa mimba kwa watoto wa kike
wengine kuacha masomo.
Ali
Shaibu mkazi wa Nakayaya alisema,jitihada zinazofanywa na Dc Mtatiro
zinapaswa kuungwa mkono na jamii ya watu wa Tunduru kwani zitasaidia
kuepusha mimba za utotoni,kupata magonjwa mbalimbali ikiwemo ukimwi na
kupoteza vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya familia na Taifa.
Awetu
Rashid, ameiomba Serikali kuendelea kuchukua hatua ya kukomesha vitendo
hivyo ambavyo kwa muda mrefu vimechangia wilaya hiyo kubaki nyuma
kielimu na hivyo kuwa maskini licha ya ukweli kwamba imebarikiwa kuwa na
rasilimali nyingi.
AfyayakoUPDATES
Comments
Post a Comment