ZIFAHAMU DALILI ZA AWALI UGONJWA WA ENDOMETRIOSIS KWA WANAWAKE

Ugonjwa wa Endometriosis ni ugonjwa wa wanawake ambao tishu zinazotengeneza ukuta wa ndani wa mfuko wa uzazi hukua sehemu ya nje ya mfuko wa uzazi. Sehemu ya ndani ya ukuta wa mfuko wa uzazi huitwa "endometrium" kwa lugha ya kimombo.

Zifuatazo ni dalili za awali za ugonjwa huu;

1. Maumivu
Maumivu makali kabla au baada ya hedhi
Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
Maumivu ya tumbo, mgongo na maeneo ya mifupa ya kiuno (pelvis)
Maumivu unapotaka kwenda kujisaidia/kwenda haja
Maumivu ya miguu

2. Hedhi
Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi, damu hiyo inaweza kuwa au kutokuwa na mabonge
Kuwa na hedhi ya muda mrefu isivyo kawaida
Kupata hedhi kabla ya muda wa kawaida

3. Uke
Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa

4. Matatizo ya Kibofu na Utumbo
Kutokwa na damu maeneo ya Kibofu au Utumbo
Kubadilika kwa hali ya utumbo i.e Kuwa na haja kubwa ngumu (constipation) na Kuharisha
Kukojoa mara nyingi isivyo kawaida

5. Kuvimba kwa tumbo wakati wa hedhi, kwaweza kuwa na maumivu au bila maumivu.

6. Kuishiwa nguvu au uchovu wakati wa hedhi
NB: Unapoona dalili hizi wahi katika kituo cha afya kilicho karibu na wewe.
#AfyayakoUPDATES

Comments