WAZIRI NDALICHAKO AZUNGUMZIA HALI ZA WANAFUNZI TOKA SHULE ZIFUNGULIWE

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, amesema kuwa tangu Kidato cha Sita, Vyuo Vikuu na vya Kati vifunguliwe Juni 1 mpaka Juni 16, hawajapokea taarifa yoyote ya mwanafunzi aliyepata maambukizi ya Virusi vya Corona.

Waziri Ndalichako amezungumza hayo wakati akitoa ratiba ya mitihani ya Darasa la 7, kidato cha pili hadi cha 4 na kusisitiza kuwa hata hizi shule zingine zinazofunguliwa Juni 29, zizingatie mwongozo uliotolewa na Wizara ya Afya juu ya namna ya kujikinga na Virusi vya Corona.

“Tangu tumefungua Shule na Vyuo Juni 1, tumekuwa tukifuatilia afya za wanafunzi wetu na mpaka Juni 16, hatujapokea kisa hata kimoja cha Mwanafunzi aliyepata Virusi vya Corona, hivyo muhimu sana kuendelea kuchukua tahadhari” Prof Ndalichako

“Darasa la 7 wataanza mitihani yao Oktoba 7-8, Kidato cha 2 wataanza mitihani yao Novemba 9 hadi Nov 20, wanaomaliza Kidato cha Nne na wa kujitegemea na wale wanaofanya mitihani ya maarifa, wataanza Novemba 23 hadi  Disemba 11, na Darasa la Nne wataanza Novemba 25 – 26, 2020″ Prof. Ndalichako
#AfyayakoUPDATES.

Comments