RAISI MAGUFULI AWATAKA DC NA DED WA JIJI LA DODOMA WAOE

“Dodoma ndio kila kitu, kwahiyo wewe Mkurugenzi (Kunambi), ni Mkurugenzi wa Jiji la Makao Makuu hata kama ni mdogo, ila utafute Mwanamke uoe, kwani hawapo Wanawake wanaotaka kuolewa na Mkugenzi jamani!?, nimekutangazia uanze kutafuta ndoa, DED unajipikia wakati Wagogo wapo wengi”-JPM

“Mkuu wa Wilaya Dodoma (Katambi) pia nae hajaoa kama DED (Kunambi), lazima tusemane hapahapa, na wewe uoe, huwezi kukaa na Viongozi wakubwa wa Makao Makuu hawana Wake, wakati Wasichana wapo wanapita hapa wengine wapo UDOM, CBE, Mipango wewe huoni tu!?”-JPM
“DC Dodoma na DED Dodoma mnataka muambiweje (ndio muoe), maana nyinyi sio Mapadri, sasa macho yenu hayaoni!?, wewe Nchimbi una Mke eeh? haya waambie hawa waoe..nilikuwa nachomekea tu kwamba tupo kwenye Makao Makuu ila tunaongozwa na Vijana ambao hawajaoa”-JPM
#AfyayakoUPDATES

Comments