MUKWEGE AJIUZULU KUONGOZA KAMATI YA KUPAMBANA NA CORONA CONGO

Mshindi wa Tuzo ya amani ya Nobel Denis Mukwege amejiuzulu wadhifa wa mkuu wa kikosikazi cha kupambana na virusi vya corona mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, akitaja matatizo ya kiutendaji, mkakati usiofanya kazi na upimaji wa polepole kama sababu za kujiuzulu kwake.

Mukwege, daktari wa afya ya uzazi nchini Congo ambaye alishinda kwa pamoja Tuzo ya Nobel 2018 kwa kazi yake dhidi ya dhulma za kingono katika vita, aliteuliwa Machi 30 kuongoza kamati ya kupambana na corona mkoani Kivu Kusini.

 Katika taarifa, amesema kumekuwa na udhaifu katika utendaji kazi na uwazi kati ya timu mbalimbali zinazoshughulika na janga hilo.

 Kwa hiyo ameamua kujiuzulu ili kuendelea kutekeleza majukumu yake ya kuwatibu wagonjwa wanaoendelea kufurika katika hospitali yake ya Panzi. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeripoti maambukizi 4,390 ya Corona, vikiwemo visa 3,980 mjini Kinshasa, na 89 Kivu Kusini na jumla ya vifo 96.
#AfyayakoUPDATES
USISAHAU KUBONYEZA SEHEMU ILIYOANDIKWA JISAJILI ILI UWE WA KWANZA KUPATA TAARIFA.

Comments