Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Zubeir bin Ally kwa niaba ya
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), ametangaza kuwa mwaka huu
hakutokuwa na ibada ya hijja hii ni kutokana na kauli iliyotolewa wiki
hii na serikali ya Saudi Arabia kutokana na janga la Corona.
Abubakar Zubeir bin Ally ameyasema hayo leo Juni 25, 2020 wakati
akiongea na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa janga la Corona
ndio limesababisha na haitakuwa kwa Tanzania pekee tu bali kwa Dunia
nzima isipokuwa waislam waliopo ndani ya Saudi Arabia.
Ameeleza kuwa BAKWATA wameunga mkono maamuzi hayo ya Saudi Arabia lengo likiwa ni kuweka usalama kwa waumini na kuwakinga na Corona kwasababu ugonjwa huo ni wa kuambukiza.
Ameeleza kuwa BAKWATA wameunga mkono maamuzi hayo ya Saudi Arabia lengo likiwa ni kuweka usalama kwa waumini na kuwakinga na Corona kwasababu ugonjwa huo ni wa kuambukiza.
Mufti Zubeir amezitaka madrasa zote nchini kuanzia sasa kurejesha
shughuli zote za madrasa nchini huku zikizingatia taratibu zote za
kiafya kama inavyoshauriwa na wataalamu wa afya nchini.
#AfyayakoUPDATES
Comments
Post a Comment