MAREKANI YASHIRIKIANA NA WHO KUHUSU EBOLA

Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema jana kuwa amefanya mazungumzo na waziri wa afya na huduma za kibinadamu wa Marekani Alex Azar kuhusu ushirikiano katika kukabiliana na mripuko mpya wa virusi vya Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hata wakati utawala wa Trump unapanga kuiondoa Marekani katika shirika hilo la afya ulimwenguni.

Mkuu wa kitengo cha kushughulikia masuala ya dharura katika shirika hilo la WHO Dkt. Michael Ryan alitaja visa tisa vya maambukizi vilivyothibitishwa katika maabara na visa vitatu vinavyoshukiwa katika mripuko huo mpya.
Mwishoni mwa mwezi uliopita, rais wa Marekani Donald Trump alisema anavunja ushirikiano wa Marekani na shirika hilo la WHO, lakini mazungumzo yanaashiria kuwa bado Marekani inaona umuhimu wa kuendelea kushirikiana nalo.
#AfyayakoUPDATES

Comments