
Magufuli amesema “Mama lishe lazima wawepo, mimi niingie nikale chakula cha mia tano badala ya elfu tano, hayo ndiyo maisha yetu ya watanzania, lakini kieleweke hiyo stendi haikujengwa kwaajili ya matajili, nimeijenga kwaajili ya watanzania wote wakiwepo maskini”
Kwa upande wa machinga amesema ” Hakuna sababu ya kuwa na stendi ya watanzania wote wa maisha yote, halafu hao hawashiriki hata kuuza zabibu hapo”
Usafiri mwingine wa daladala na pikipiki Rais amesema ” Nilazima jiji litengeneze mazingira, watu wa daladala wawe wanaweza kufika pale, wa bodaboda waweze kufika pale, wa pikipiki waweze kufika pale, ili kusudi hata mvua ikiwa inanyesha mtu asianze kutembea na mizigo yake, wapo wengine wagonjwa..”
Aidha ametoa onyo kwa walinzi waliopewa kazi kwenye stendi hiyo kutoka Suma JKT kuacha kuwarusha watu vichura na kufanya kazi ya kuwalinda, kama wanavyofanya mikoa mingine “Hapo sio jeshini…hawakuajiliwa pale kuwapigisha vichura” Amesisitiza JPM.
Kwa upande wake Mkurugenzi, Kunambi ameahidi kufanyia kazi maelekezo
yote yaliyotolewa ndani ya muda mfupi na kuwatafutia vijana mikopo kama
ambavyo Rais ameagiza.
#AfyayakoUPDATES
Comments
Post a Comment