MAGUFULI: "MSIWADHARAU HAWA WAMETUEPUSHA NA CORONA, WIZARA ONGEZENI BAJETI YAO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli leo June 11, 2020 akizindua Jengo la TARURA amemshukuru Mungu kwa kutuepusha na ugonjwa wa Virusi vya Corona.

“Tunamshukuru Mungu kwa kutuepusha na ugonjwa huu wa corona mambo sasa yanaenda vizuri, tusidharau dawa za mitishamba uchawi tu ndio mbaya lakini miti yote iliumbwa kwa ajili ya kutusaidia sisi, dawa za kienyeji ni tiba kama zilivyo dawa nyingine tulipumbazwa tu kwamba tusiamini kilicho chetu tuamini kilicho chao sasa tubadilike,” JPM
#AfyayakoUPDATES

Comments