Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba,
amekitaka chama cha ACT wazalendo kurejesha ofisi za majengo ya CUF
walizozipora na kuzibadilisha rangi na kuzifanya za kuwa ACT kwani
kufanya hivyo ni kinyume cha sheria ya vyama vya siasa.
Profesa Lipumba ameyasema hayo wakati akiwa kwenye ziara yake Visiwani
Pemba, ambapo alisema chama cha siasa kupora ofisi za chama kingine cha
siasa ni kuvunja sheria ya vyama vya siasa.
''Ni bora ofisi za majengo ya CUF waliyoyahodhi na kuyapaka rangi za ACT Wazalendo wazirejeshe kwani hali hiyo inaweza kuwasababishia adhabu kubwa dhidi ya kupora ofisi hizo'', amesema.
''Ni bora ofisi za majengo ya CUF waliyoyahodhi na kuyapaka rangi za ACT Wazalendo wazirejeshe kwani hali hiyo inaweza kuwasababishia adhabu kubwa dhidi ya kupora ofisi hizo'', amesema.
Aidha Profesa Lipumba amesema vyama vya siasa visiwe chanzo cha uadui na
badala yake wafanye siasa za kisasa na kushindana kwa hoja kuwa nani
anayeweza kutumia wananchi vizuri zaidi kwani katiba ya umoja wa kitaifa
inawapa fursa ya kuweza kutekeleza Sera zao.
#AfyayakoUPDATES
Comments
Post a Comment