IJUE SABABU YA DENI LA SERIKALI KUFIKIA TRILION 55.43

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango, amesema kuwa deni la Serikali lilichangiwa na kupokelewa kwa mikopo mipya ya kugharamia miradi ya maendeleo inayochochea kasi ya ukuaji wa uchumi.
Waziri Mpango ameyabainisha hayo leo Juni 11, 2020, Jijini Dodoma katika Mkutano wa 19, Kikao cha 43, alipokuwa akitoa taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2019 na kuongeza kuwa hata hivyo deni la Serikali bado ni himilivu.

"Hadi Aprili 2020 Deni la Serikali lilifikia Tril 55.43, kati ya kiasi hicho deni la nje lilikuwa Tril 40.57, na deni la ndani ni Tril 14.85, Deni la Serikali lilichangiwa na kupokelewa kwa mikopo mipya ya kugharamia miradi ya maendeleo inayochochea kasi ya ukuaji wa uchumi, matokeo ya tathimini ya uhimilivu wa deni uliofanyika Disemba 2019, imeonesha kuwa deni la Serikali ni himilivu katika kipindi cha muda mfupi wa kati na mrefu" amesema Waziri Mpango.

Aidha akizungumzia suala la upatikanaji wa pato la kila mtu, Waziri Mpango amesema kuwa, "Mwaka 2019 Pato la Wastani la kila mtu lilikuwa Mil 2. 5, ikilinganishwa na Mil 2.4 mwaka 2018 sawa na ongezeko la 5.1%, vilevile Pato la Wastani kwa kila mtu kwa Dolla za Marekani liliongezeka hadi kufikia Dolla 1, 121 mwaka 2019, kutoka Dolla 1,078 mwaka 2018".
#AfyayakoUPDATES

Comments