Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imetangaza rasmi kumalizika
kwa janga la ugonjwa wa Ebola ambao ulizuka katika eneo la mashariki mwa
nchi hiyo Agosti mwaka 2018 na kusababisha vifo vya watu 2,277.
Waziri wa afya wa nchi hiyo Eteni Longondo alisema kuwa kuzuka kwa ugonjwa huo, kulidumu kwa mrefu zaidi, pamoja na ugumu wa matibabu na wa hatari, katika historia ya miaka 60 ya nchi hiyo.
Eneo la mashariki mwa nchi hiyo limeadhimisha rasmi kumalizika kwa ugonjwa huo uliodumu kwa karibu miaka miwili wakati makundi yenye silaha na jamii kutokuwa na imani kulivuruga ahadi za kuwa na chanjo mpya.
Tukio hilo la leo limegubikwa na changamoto nyingi za kiafya ambazo bado
nchi hiyo inakabiliana nazo, kubwa zaidi ikiwa ni janga la ugonjwa wa
surua, ongezeko la kitisho cha ugonjwa wa COVID-19 pamoja na kuzuka upya
kwa ugonjwa wa Ebola upande wa kaskazini.
#AfyayakoUPDATES
Comments
Post a Comment