BRAZIL YASHIKA NAFASI YA PILI KWA VIFO VYA COVID-19 DUNIANI

SAO PAULO,Wizara ya afya ya Brazil imerekodi jumla ya vifo 41, 828 katika kipindi hiki cha janga la virusi vya corona, ikimaanisha kwamba sasa imezidi idadi ya vifo ya nchini Uingereza. Brazil sasa inashika nafasi ya pili ya idadi ya vifo vilivyotokana na janga hilo duniani. Rekodi hizo ni kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha John Hopkins cha Marekani.

 Hapo jana maafisa nchini humo wamerekodi jumla ya vifo 909 katika kipindi cha masaa 24. Ni taifa ambalo limeathiriwa vibaya zaidi katika eneo la Amerika ya Kusini kwa kuwa na maambukizi 828,000.

Taarifa hizo mpya zinatolewa katika kipindi ambacho Brazil imeanza kupunguza vizuizi, vilivyowekwa miezi miwili iliyopita katika kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona.

Katika jiji la Sao Paulo ambalo ndilo kitovu cha janga hilo, maduka ya kawaida na yale makubwa kabisa yameruhusiwa kufunguliwa kwa masaa manne kwa siku. Na katika miji midogo kumekuwa na misongamano ya watu madukani.
#AfyayakoUPDATES

Comments