
Ameongeza kuwa ni Dhahiri kuwa ugonjwa wa COVID 19 ni ugonjwa mpya ulimwenguni ambao kila nchi imechukua hatua na afua ambazo zinaendana na hali halisi,mazingira ya nchi husika na kupongeza msimamo wa Tanzania na hatua zinazoendelea kuchukuliwa katika kupambana na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kutoa tahadhari kwa wananchi kufuata muongozo wa wataalam wa afya.
Kwa upande wake Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amemshukuru Waziri huyo wa Norway kwa kutambua jitihada za Tanzania katika kupambana na virusi vya corona licha ya baadhi ya nchi kubeza muongozo wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa kuweka zuio la kutoka nje (lockdown).
Pia ameishukuru Norway kwa kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania
katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na masuala ya kidiplomasia na
maendeleo hususani katika kusaidia jitihada za kupambana na mabadiliko
ya tabianchi na kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia malengo yake katika
utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu.Mazungumzo baina ya Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba
John Kabudi na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway Bw.
Dag-IngeUlstein yamefanyika katika Ofisi za Wizara za Jijini Dodoma kwa
lengo la kuimairisha mahusiano baina ya nchi hizo pamoja na
kubadilishana uzoefu katika kupamabana na virusi vya corona.
#AfyayakoUPDATES
SUBSCRIBE NA SHARE BLOG HII
Comments
Post a Comment