AJALI ILIYOHUSISHA MAGARI MANNE YAUA MMOJA MBEYA

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani Jijini Mbeya, ikihusisha magari manne na bajaji mbili katika eneo la Mbembela.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema chanzo cha ajali ni gari kubwa la mafuta lenye namba T 329 BHS, kufeli breki na kuyagonga magari mengine ikiwemo gari la abiria na kusababisha kifo cha dereva wa gari hiyo.
#AfyayakoUPDATES

Comments