AFRIKA YATAKA UN IJADILI UBAGUZI WA RANGI

Mataifa ya Afrika yamelitaka Baraza la Haki za Binaadamu la UN kujadili kwa dharura ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi katika kipindi hiki ambacho Marekani na maeneo mengine ya ulimwengu yakigubikwa na maandamano.

Katika barua yake iliyoandikwa kwa niaba ya mataifa 54 ya Afrika, Balozi wa Burkina Faso katika Umoja wa Mataifa mjini Geneva amekitaka chombo cha juu kabisa cha usimamizi wa haki za binaadamu kuanzisha mjadala wa dharura utakaojikita katika ukiukwaji wa haki za binadamu unaochochewa kwa ubaguzi wa rangi, ukatili wa polisi dhidi ya watu wa asili ya Kiafrika na ukandamizaji dhidi ya maandamano ya amani ambayo yanashinikiza haki za msingi ziheshimiwe.

Barua hiyo ambayo ameandikiwa rais wa baraza hilo Muastria, Elisabeth Tichy-Fisslberger, imetaka mjadala huo kufanyika wiki ijayo, pale ambapo mkuatano wa 43 wa baraza hilo utakapoanza tena baada ya kusitishwa mwezi Machi, kutokana na kuzuka kwa janga la COVID-19. Wito huo unatolewa baada ya wiki hii familia yaFloyd, pamoja na familia za waathirika wengine wa matumizi ya nguvu ya polisi na zaidi ya asasi za kiraia 600 kulitoa wito baraza hilo, kutoa nafasi ya udharura katika kushughulikia ubaguzi wa kimfumo na hali ya polisi kushindwa kuwajibika nchini Marekani.

Ili baraza hilo lilizingatie ombi la namna hiyo, lazima liwe na uungwaji mkono wa japo taifa moja, na kwa vile limetolewa na kundi kubwa la mataifa, imeongeza nafasui kubvwa kupata nafasi ya kujadililiwa. Barua hiyo hiyo iligusia kisa cha George Floyd, aliyekuwa na umri wa miaka 46, kijana mwenye asili ya Kiafrika ambae alifariki dunia akiwa mikononi mwa polisi huko Minneapolis, baada ya polisi mzungu, ambae baadae alishitakiwa kwa kesi ya mauwaji, kumkandamiza kwa goti lake shingoni kwa karibu dakika tisa.  Kisa hicho ambacho baadae kilitapakaa duniani kote kwa njia ya video kimezuisha maandamabo makubwa Marekani na maeneo mwengine ya ulimwengu.
#AfyayakoUPDATES

Comments