WATOTO MILLIONI 86 WENGINE HATARINI KUWA MASIKINI KUTOKANA NA CORONA DUNIANI

Mashirika mawili ya kimataifa ya kuwahami watoto wadogo yametahadharisha kuhusu hatari ya watoto miliioni 86 wengine kutumbukia kwenye umaskini kutokana na maambukizi makubwa ya ugonjwa wa corona duniani.
Kanali ya talevisheni ya "RT al Arabi" imenukuu uchunguzi wa karibuni kabisa wa Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (Unicef) na Shirika la Kimataifa la Kuwaokoa Watoto (Save the Children) ukionesha kuwa, madhara ya kiuchumi ya ugonjwa wa corona yatawafanya watoto wengine milioni 86 kuwa maskini ifikapo mwishoni mwa mwaka huu wa 2020

Jana Alkhamisi, mashirika hayo mawili ya kimataifa yalitoa tamko la pamoja kuhusu uchunguzi wao unaoonesha kuwa, ifikapo mwishoni mwa mwaka huu wa 2020 watoto wanaoteseka kwa njaa duniani wataongezeka na kufikia milioni 672 na kiwango hicho kitakuwa ni ongezeka la asilimia 15 ikilinganishwa na mwaka jana 2019.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa mashirika hayo, thuluthi mbili ya watoto hao wanaishi katika maeneo ya kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika na kusini mwa bara la Asia.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na kwa kutegemea data za jamii za karibu nchi 100 duniani, watoto wapya watakaoteseka na umaskini kutokana na ugonjwa wa COVID-19 watakuwa wengi wao ni kutoka barani Ulaya na Asia ya Kati kuliko maeneo mengine yote duniani.
#AfyayakoUPDATES

Comments