SERIKALI YAKANUSHA MARUFUKU YA KUVAA BARAKOA


Serikali ya Tanzania imekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao zikidai kuwa Rais John Magufuli amepiga marufuku uvaaji wa barakoa za wananchi kutokana na kupungua kwa wagonjwa nchini wa COVID-19.
Katika ujumbe uliotumwa kwenye mtandao wa twitter wa mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu Gerson Msigwa amesema taarifa hiyo ni uzushi na ni ya kupuuzwa.

Comments