Serikali ya Afrika Kusini imesema kuanzia Jumatatu itawaruhusu watu
kununua pombe na kuhudhuria makanisani ikiwa ni sehemu yake ya kulegeza
masharti ya kukabiliana na janga la corona. Lakini hatua hizo zitakwenda
sambamba na kanuni za kujikinga katika taifa hilo lenye visa vingi vya
maambukizi barani Afrika.
Uuzaji wa vileo, ambao ulipigwa marufuku tangu Machi 27, utaruhusiwa
kwa siku nne kwa wiki. Lakini hakuna pombe ambayo itakayoruhusiwa
kununuliwa Ijumaa na katika siku za mapumziko ya nyuma, na baa pia
zitaendelea kufungwa.
Na pombe hizo zitanywiwa nyumbani tu. Makanisa yatafunguliwa lakini
kusiwe na mkusanyiko wa watu wanaozidi 50. Vitakasa mikono, barakoa na
kujitenga baina ya mtu na mtu ni mambo ya lazima kanisani. Afrika ya
Kusini ina maambukizi 25, 937 huku vifo vikiwa 552.
#AfyayakoUPDATES
Comments
Post a Comment