KUHUSU MIKOPO PESA IPO TAYARI

“Kuhusu mikopo hapa JPM alizungumza kwa msisitizo kwamba hataki vijana wake wapate usumbufu, niwahakikishie fedha tayari zipo, ikifika May 28 vyuo viwe vimewasilisha nyaraka muhimu ili wanafunzi wakiripoti vyuoni Bodi ya Mikopo iweze kutoa fedha”-Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako

“Nivikumbushe vyuo kuwa pamoja na kufungua tuendelee kuchukua tahadhari, maambukizi ya corona yamepungua ila kama Rais alivyosema ugonjwa haujaisha, hivyo wanafunzi wanaporudi shuleni wasije kuwa sababu za kurudisha mlipuko, tahadhari zichukuliwe ”-NDALICHAKO

“Nimeongea na Waziri wa Afya tunaandaa muongozo wa ziada ambao tutaupeleka katika kila shule na vyuo ili kuhakikisha tahadhari dhidi ya corona zinaendelea kuchukuliwa, viongozi wa vyuo simamieni tahadhari za afya ili tujikinge na corona” -NDALICHAKO

“Tumepokea maelekezo ya kufungua vyuo kwa furaha maana Wizara ya Elimu bila wanafunzi kuwa shuleni kiukweli tulikuwa tumepooza sana, sasa mtatuona maana tulikuwa kimya, tumejipanga, tutakwenda kuangalia jinsi vyuo vilivyojipanga kuwapokea wanafunzi”-NDALICHAKO
#AfyayakoUPDATES

Comments