FORM SIX KUANZA MITIHANI JUNE 29

“Tumepokea maelekezo ya Rais JPM na tumejipanga kuyatekeleza, kidato cha sita tunawaelekeza kufanya maandalizi ili wanze masomo June 01,2020, wanafunzi wa shule za bweni kuanzia May 30,2020 wanaweza kwenda shule ili June 01,2020 waanze masomo”-Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako

“Mitihani ya kidato cha sita itaanza rasmi June 29 hadi July 16, 2020 na mitihani hii ya kidato cha sita itaenda sambamba na mitihani ya ualimu, natoa wito kwa Baraza la Mitihani kuhakikisha wanasambaza ratiba ya mitihani hii mapema”- NDALICHAKO

“Tumeliagiza Baraza la Mitihani kuhakikisha mitihani ya kidato cha sita inapomalizika ni lazima matokeo yatoke kabla ya August 31,2020 ili tuendane na maagizo ya JPM kwamba hawa wanafunzi waweze kujiunga na vyuo vikuu kama ambavyo ilikuwa imepangwa”-NDALICHAKO

“Vyuo Vikuu viweke utaratibu wa kuhakikisha masomo yanaendeshwa kwa mfumo wa kufidia muda uliopotea likizo ya corona, ratiba zibadilike kuwe na muda zaidi wa kusoma,ifikapo tarehe 27 utaratibu uwe umewasilishwa TCU na NACTE ili tujue wamepanga nini”-NDALICHAKO
#AfyayakoUPDATES

Comments