FAIDA ZA KULA ILIKI KIAFYA


Wapishi wengi wanapenda kutumia iliki kwa kuwa inaongeza radha na harufu nzuri kwenye vyakula.
Hata hivyo, pamoja na kuchochea harufu nzuri pia ina virutubisho vingi ikiwa ni pamoja na vitamini A na C, madini ya calcium, potassium, sodium, copper, zinc na magnesium.

Kwa mujibu wa kitengo cha Kilimo na Lishe cha Marekani, kinasema iliki ina carbohydrates gram 68, protini 11 na nyuzinyuzi gramu mbili.

Pia inaipa figo uwezo wa kuondoa taka mwili na kusaidia kuweka sawa mfumo wa mmeng'enyo wa chakula tumboni.

Iliki pia inasaidia kuondoa hali ya kiungulia na gesi tumboni na tatizo la kukosa choo.

Saga iliki kisha tumia unga wake kijiko kimoja cha chakula katika maji moto yaliyo katika kikombe cha chai. Kunywa kila siku muda wa wiki mbili utaona matokeo mazuri katika mwili wako.

Utafiti mwingine uliofanywa na Chuo cha Pharmacy of King Saud kilichoko Said Arabia ulibaini kuwa iliki ina uwezo mkubwa wa kuboresha mishipa ya damu kwenye moyo na hivyo kuulinda dhidi ya magonjwa mbalimbali ya mfumo wa moyo.

Iliki pia inaondoa maradhi ya kinywa kinachotoa harufu mbaya na kutibu vidonda vya mdomoni.

Tumia unga wa iliki uliochanganywa na maji ya uvuguvugu kisha sukutua mdomoni kila siku asubuhi na jioni muda wa wiki tatu.

Kiungo hiki pia ni msaada kwa wenye maamhukizi katika njia ya mkojo magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana.

Tumia kijiko kimoja cha unga wa iliki katika uji usio mzito katika kikombe cha chai kila siku muda wa wiki mbili.

Iliki pia inasaidia kukinga saratani na shinikizo la damu iwapo utatumia kwa kuzingatia maelekezo kutoka kwa wataalamu wa afya.

Pia ina uwezo wa kuondoa tatizo la pumu katika hatua za awali na inapochanganywa na mdalasini inasaidia kupunguza maumivu ya koo.



Comments