CORONA: US KUIPA TZ BILIONI 5.6


Marekani imetangaza kuwa kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) itaongeza USD 2.4 M (Tsh. Bil. 5.6) ikiwa ni msaada kwa sekta ya afya kuimarisha uwezo wa maabara na upimaji wa kimaabara, jitihada za utoaji taarifa na miradi mingine mbalimbali.
 •
Taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani leo imesema fedha hizi ni nyongeza ya msaada wa USD milioni moja unaolenga kusaidia mapambano dhidi ya kirusi corona uliotolewa hivi karibuni hivyo kufanya kiasi kipya cha pesa zilizotolewa kwa Tanzania kukabiliana na corona kufikia USD milioni 3.4.

Taarifa hiyo imesema kiasi kingine cha dola za kimarekani milioni 1.9 zilibadilishwa matumizi na kuelekezwa kwenye mapambano dhidi ya corona na kufanya jumla ya pesa zilizotolewa na Marekani katika kukabiliana na corona Tanzania hadi sasa kufikia jumla ya USD milioni 5.3 (Bilioni 12 Tsh. ) via @usembassytz

Comments