CORONA: BENDERA NUSU MLINGOTI

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa amri jana ya bendera kushushwa nusu mlingoti kwa siku tatu mfululizo, kuomboleza vifo vya Wamarekani zaidi ya Elfu 96 waliofariki Dunia kutokana na virusi vya corona.

Rais Trump ameamrisha bendera kushushwa nusu mlingoti Marekani kama ishara ya kuwakumbuka waliofariki kwa corona ila bendera zitabakia nusu mlingoti Jumatatu ijayo ambayo ni Siku ya Mashujaa ya kuwakumbuka waliopoteza maisha wakilitumikia jeshi la Marekani.
(via @dw_kiswahili )

Comments