CHANJO DHIDI YA COVID-19 YAANZA KUFANYIWA MAJARIBIO AUSTRALIA

Mkurugenzi wa Utafiti wa kampuni ya biotechnology Novavax, yenye makao makuu nchini Marekani Gregory Glenn katika mkutano uliofanyika kupitia video, ametangaza kwamba awamu ya kwanza ya jaribio la chanjo imeanza na watu kadhaa wamejitolea nchini Australia.

Katika wigo wa hatua ya kwanza, Glenn amesema kuwa chanjo inayoitwa "NVX-CoV2373" itatumika kwa watu 131 waliojitolea na kwamba usalama wa chanjo hiyo utapimwa na athari zake zitazingatiwa.

Glenn ameendelea kwa kusema kuwa Novavax inaweza kutengeneza dozi angalau milioni 100 mwaka huu na bilioni 1.5 mnamo 2021.

Katika taarifa iliyotolewa na Novavax, inatarajiwa kwamba matokeo ya majaribio ya chanjo huko Melbourne na Brisbane yanatarajiwa Julai.

Awamu ya pili inatarajiwa kuchukua nafasi baada ya mwezi Julai kwa maelfu watakaoshiriki katika nchi tofauti.
#AfyayakoUPDATES

Comments