ULAJI UNAOFAA KWA MAKUNDI


Ulaji bora unatakiwa kuzingatia mahitaji ya mwili kutokana na jinsi, umri, mzunguko wa maisha, kazi na hali ya afya.

WATOTO
  • Chini ya miezi 6 wapewe maziwa ya mama pekee.
  • Miezi 6 hadi 2, watoto wapewe maziwa ya mama na chakula mchanganyiko. Kama mtoto hanyonyi maziwa ya mama, anahitaji kupewa maziwa mengine angalau nusu lita kwa siku na chakula mchanganyiko.
  • Miaka 2 mpaka 5, watoto wale angalau milo mitano kwa siku na maziwa yaendelee kuwa sehemu ya mlo wa mtoto.
  • Miaka 6 hadi 9 wapewe milo kamili mitatu na vitafunwa mara 2 au 3 kwa siku.

VIJANA
  • Vijana (wavulana na wasichana) wanahitaji virutubishi kwa wingi zaidi kwani wanakua haraka hivyo ni muhimu kuongeza kiasi cha chakula.
  • Wasichana wanahitaji madini chuma kwa wingi kwasababu hupoteza damu wakati wa hedhi, hivyo wale vyakula vyenye madini chuma, asidi ya foliki na vitamini C kwa wingi ili kutengeneza chembe chembe za damu kwa wingi.

NB. Inashauriwa pia watumie chumvi yenye madini joto.

WAZEE
  • Wanahitaji milo kamili midogomidogo mara nyingi kwa siku.
  • Wale vyakula laini vyenye virutubishi kwa wingi.
  • Wale vyakula vyenye madini ya chokaa kwa wingi kama maziwa na dagaa.
  • Waongeze ulaji wa vyakula vyenye makapi mlo kwa wingi.

MWANAMKE MJAMZITO
  • Ushauri kuhusu ulaji unaofaa uliotolewa hapo juu unawahusu watu wote wakiwemo wanawake wajawazito. Zaidi ya hayo, mwanamke mjamzito anahitaji kuongeza chakula kukidhi mahitaji yake binafsi na ya mtoto aliye tumboni. Vinginevyo anaweza kupatwa na matatizo yafuatayo;
  • Upungufu wa damu kutokana na upungufu wa madini chuma mwilini - hii ni sababu kubwa ya ya vifo vya wanawake wakati wa ujauzito na kujifungua.
  • Ukosefu wa madini joto - unaweza kusababisha mimba kuharibika, kuzaa mtoto mfu, udumafu wa mwili na akili kwa watoto na vifo vya watoto wachanga.
  • Kutoongezeka uzito kwa kiasi cha kutosha - hii husababisha watoto kuzaliwa na uzito upungufu na kuwaweka kwenye hatari kubwa ya kushambuliwa na magonjwa.
  • Hivyo wanawake wajawazito licha ya ushauri kuhusu ulaji unaofaa, wanashauriwa;
  • Kutumia vidonge vya madini chuma, vidonge vya asidi ya foliki, vidonge vya kutibu minyoo, dawa za kuzuia malaria na vyandarua vilivyowekwa viuatilifu ili kujikinga na malaria vyote hivyo ili kuzuia upungufu wa damu.
  • Kutumia chumvi yenye madini joto.
  • Kujua hali ya VVU ili kushauriwa njia salama za kumlisha mtoto.
  • Kufikiria njia ya uzazi wa mpango atakayochagua ili kupata muda wa kulea mtoto na kumwezesha kuwa na afya nzuri.

PEMBE TATU YA ULAJI UNAOFAA

MWISHO
 Asante kwa kuendelea kufuatilia blog yako pendwa ya AFYA YAKO, kwa leo tunaishia hapa katika somo letu la ulaji unaofaa. kwa maswali na maoni comment hapo chini utapata majibu, tukutane kwa wakati mwingine 😍😍😍
NAWA MIKONO UWAKINGE WENGINE
TANZANIA BILA CORONA INAWEZEKANA

Comments