SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI

SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI INAZUILIKA.


  • Mlango wa kizazi ni kiungo katika tumbo la uzazi la mwanamke.
  •  Saratani ya mlango inasababishwa na na virusi vijulikanavyo kitaalam kama Human Papilloma Virus (HPV).
  • Saratani ya mlango wa kizazi ni ugonjwa hatari na unaua wanawake wengi hasa nchi zinazoendelea.
  • HPV huambukizwa kwa ngono toka kwa mtu mwenye virusi hivyo. Kwa jamii zile zinazofanya ngono kinyume na maumbile virusi hivi pia huambukiza sehemu ya haja kubwa/koo.
  • Kila mtu akianza kushiriki ngono anakuwa katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya HPV.
  • Tafiti zinaonesha kuwa, katika kila wanawake wanne wanaoshiriki ngono watatu(3) wanapata maamukizi ya HPV wakati fulani wa maisha yao.
  • Wasichana wenye umri mdogo wanao uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya HPV.
                                     DALILI ZA MAAMBUKIZI YA HPV
  1. Baadhi ya dalili za awali za maambukizi ya HPV ni uvimbe kwenye sehemu za uke au uume;(au koo/haja kubwa )vijulikanavyo kama viotea.
  2. Dalili za baadae ni mabadiliko katika seli za mlango wa kizazi, ambazo ni dalili za awali za saratani ya mlango wa kizazi.
  3. Mabadiliko haya yasipodhibitiwa mapema hugeuka kuwa saratani ya mlango wa kizazi.
DALILI ZA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI                 
Awali saratani ya mlango wa kizazi haina dalili. Hugundulika tu kwa kuchunguzwa na wataalamu wa afya. Dalili zake ni:
  • Kutokwa na uchafu na / au damu kwenye uke.
  • kupata hedhi bila mpangilio maalumu.
  • kutokwa na damu ukeni baada ya tendo la ngono
CHANJO YA KUKINGA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI (HPV-VACCINE)
  1. Chanjo ya HPV inakinga maambukizi ya virusi vya  HPV vinavyosababisha saratani ya mlango wa kizazi.
  2. Chanjo ya HPV inatolewa mara mbili ili kupata kinga kamili.
  3. Chanjo hii inaweza kupunguza matukio ya saratani ya malango wa kizazi kwa kiwango kikubwa.
  4. Chanjo hii ni salama na imethibitishwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto na Shirika la Afya Duniani(WHO)
Image result for dalili za saratani ya shingo ya kizazi
  • Chanjo hii inatolewa na watumishi wa vituo vya kutolea huduma za afya na huduma za mkoba na mashuleni.
  • Chanjo hii inatolewa kwa wasichana waliofikisha umri wa miaka kumi na nne (14).
  • Ili kupata dozi kamili, walengwa watahitaji kupata dozi mbili (2)
  • Dozi ya pili itatolewa miezi 6 baada ya kupata dozi ya kwanza.
MUHIMU: Ni muhimu kukamilisha dozi zote ili kupata kinga kamili
  • Chanjo hii inatolewa bila malipo
  • Chanjo hii ni salama
CHANJO NI HAKI YA KILA MSICHANA MWENYE UMRI WA MIAKA 14.                                HAKIKISHA BINTI YAKO ANAPATA CHANJO.



Comments