MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA

MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA.
Leo tuangalie nini maana ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni magonjwa ambayo hayaambukizwi na mtu mwingine kwa kuwa hakuna vimelea mwilini vinavyohusiana na magonjwa hayo.
> Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni kama ya;
i. Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu
ii. Figo
iii. Saratani
iv. Kifua sugu
v. Kisukari
vi. Magonjwa ya akili
vii. Ugonjwa wa selimundu(sickel cell)
> Mwaka 1999, magonjwa yasiyo ya kuambukiza yalikadiriwa kuchangia karibu 60% ya vifo vyote duniani na asilimia 43% ya ukubwa wa tatizo la magonjwa duniani.
>Tatizo la magonjwa yasiyo ya kuambukiza linakua kwa kasi katika nchi zinazoendelea, kama Tanzania.
 >Mambo yanayochangia kuongezeka kwa magonjwa haya ni mabadiliko ya taratibu za kimaisha zinazohusisha matendo yanayoweza kusababisha ugonjwa.
 >Taratibu hizo za kimaisha zinazosababisha magonjwa hayo ni;
i. Kutofanya mazoezi: Kukaa sehemu moja muda mrefu bila kutembeatembea, kutoshiriki michezo, kuangalia runinga kwa muda mrefu.
ii. Ulaji usiofaa: Kula chakula kuzidi mahitaji ya mwili na hivyo kunenepa, kula mafuta na chumvi zaidi ya mahitaji ya mwili, Kutokula mbogamboga na matunda kiasi cha kutosha, Kula nafaka zilizokobolewa.
iiiMatumizi ya pombe
ivMatumizi ya tumbaku na madawa ya kulevya.
v. Msongo wa mawazo.
Itaendelea katika makala ijayo………….
ASANTENI
Usisahau comment, like na share kwa wengine ili waweze kupata elimu hii.

Comments