KUGUNDUA NA KUZUIA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA


Karibuni tena katika muendelezo wa somo lililopita lililokuwa linahusu MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZWA na tukaishia kipengele cha TARATIBU ZA KIMAISHA ZINAZOSABABISHA MAGONJWA HAYO.
Sasa tuangalie kipengele cha KUGUNDUA NA KUZUIA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA.

Ø Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanaweza yakawa bila dalili zozote kwa miaka kadhaa ya kuwa na ugonjwa huo japokuwa mwili utakuwa umeshaathirika sana.
Ø Kwa mfano mtu anaweza kuishi miaka mingi na shinikizo la damu bila dalili zozote hadi pale anapopata kiharusi, moyo unaposhindwa kufanya kazi au figo zinapokuwa zimeharibika kwa sababu ya msukumo huo wa damu
Ø Ugonjwa wa kisukari unaweza usiwe na dalili za kumfanya mtu atafute tiba hadi pale macho, figo, moyo au mishipa ya damu au fahamu inapokuwa imeharibika vibaya na kusababisha dalili.
Ø Katika uatafiti uliofanywa mwaka 2012 nchini Tanzania ulioshirikisha watu wenye umri wa miaka 25 na kuendelea, kwa kila watu 14 waliokutwa na shinikizo la damu, ni mmoja tu kati ya hao ndiye aliyekuwa amegunduliwa tayari.
Ø Kwa upande wa kisukari, ni chini ya nusu ya wote waliokutwa na ugonjwa ndio waliokuwa wamegunduliwa.
Ø Hivyo inashauriwa watu wote kupata uchunguzi wa mara kwa mara ili kugundua kuwepo kwa magonjwa haya.
Ø Tiba ya mapema inapunguza uwezekano wa kupatwa na madhara zaidi.
Ø Kwa magojwa mengine kama vile saratani, tiba ya mapema inaweza kuondoa ugonjwa huu moja kwa moja.

Magonjwa yanayoshauriwa kuchunguzwa mara kwa mara ni:
Ugonjwa wa kisukari
Ugonjwa wa shinikizo la damu
Magonjwa ya macho kwa watoto na watu wazima
Ugonjwa wa selimundu
Saratani ya matiti

DALILI ZINAZOWEZA KUASHIRIA KUWEPO KWA MAGONJWA YASIYOYA KUAMBUKIZA.
Kwa watu wazima, mara moja kila mwezi pitia orodha hii na pata ushauri wa mtaalamu wa afya ikiwa una dalili mojawapo:
Kupungua uzito bila sababu.
Kuchoka bila sababu
Kichwa kuuma.
Kuona kizunguzungu.
Kutoona vizuri, kuona giza au kushindwa kusoma.
Makengeza kwa watoto wenye umri chini ya miaka 6
Ganzi ya meno, meno kucheza/kung’oka, kutika damu kwenye fizi.
Ganzi au maumivu (kuwaka moto) kwenye mikono na miguu.
Maumivu ya kifua hasa wakati unajishughulisha
Kupumua kwa shida au kukosa pumzi baada ya kujishughulisha tu kidogo.
Kukosa pumzi usiku wakati umelala
Moyo kwenda haraka.
Kubadilka tabia ya choo(kufunga choo)
Kukojoa mara kwa mara au mkojo kuchelewa kutoka.
Kutokwa damu sehemu yoyote(pua, makohozi ya damu, choo kubwa, mkojo, ukeni)
Kutoka damu nje ya mzunguko wa hedhi, wakati wa tendo la ndoa au baada ya kufunga hedhi.
Kutokwa na maji maji au ute ukeni, uwe au usiwe na harufu/rangi yoyote.
Vidonda visivyopona.
Kujisikia huzuni/upweke, woga, wasiwasi.
Hasira nyingi.
Kunywa pombe kwa wingi.
Kuvuta sigara kwa wingi
KUMBUKA
Ajali nazo ni magonjwa yasiyo ambukiza.
Usiendeshe gari kama umekunywa muda si mrefu na pombe bado ipo mwilini.
Vaa mkanda kila unapokuwa kwenye gari.
Vaa kofia ngumu kila unapopanda pikipiki.
Zima na usiinue simu wakati unaendesha.
Pima macho yako kila mwaka.
Vaa koti unapoendesha pikipiki.
MWISHO
Tukutane wakati mwingine kwa sasa tunaishia hapa, somo lijalo litakuwa linahusu ULAJI UNAOFAA NA MTINDO BORA WA MAISHA usikose. Endelea kutembelea facebook page ya AFYA YAKO @lindaafyayakoo na blog ya AFYA YAKO https://lindaafyayako.blogspot.com/

Comments