KIHARUSI

Leo tuangalie KIHARUSI ni nini?
KIHARUSI ni ugonjwa wa ghafla unaotokana na ubongo kukosa hewa na virutubishi kwa sababu ya kuziba au kupasuka kwa mishipa ya damu inayosambaza damu kwenye ubongo. Msukumo mkubwa wa damu unaweza kusababisha kupasuka kwa mishipa ya damu. Mafuta mengi yanaweza kuganda na kuziba mishipa ya damu.

                                                      DALILI ZA KIHARUSI
  • Kulemaa ghafla uso, mkono au mguu mara nyingi ikiwa ni upande mmoja tu wa mwili.
  • Kushindwa kuongea vizuri au kuelewa au kufahamu kinachoendelea.
  • Shida kuona jicho moja au yote mawili.
  • Shida kutembea, kizunguzungu, 
  • Maumivu makali ya kichwa ya ghafla bila sababu inayoeleweka

VITU VINAVYOONGEZA UWEZEKANO WA KUPATA KIHARUSI

  • Msukumo mkubwa wa damu
  • Uvutaji wa sigara.
  • Magonjwa ya moyo.
  • Ulaji usiofaa.
  • Mazoezi hafifu.
  • Ugonjwa wa kisukari.
NJIA ZA KUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUPATA KIHARUSI.

  • Punguza chumvi na mafuta kwenye vyakula.
  • Usivute sigara 
  • Epuka vyakula vya kukaanga.
  • Kula matunda na mbogamboga kila siku.
  • Fanya mazoezi ya mwili angalau kwa nusu saa kila siku.
  • Usinywe pombe kwa wingi.
NB: Unapomuona mtu ana dalili za kiharusi unashauriwa kumpeleka haraka hospitali kwa ajili ya matibabu.
MWISHO
Huo ndio mwisho wa somo letu lililokuwa linahusiana na KIHARUSI. Katika somo lijalo tutaweza kuona ULAJI UNAOFAA NA MTINDO BORA WA MAISHA ili kujikinga na magonjwa kama haya.

Usisahau ku comment na ku share kwa wengine ili kuweza kusambaza elimu hii kwa wengi zaidi

Comments