HOMA YA KIRUSI CHA KORONA

ELIMU KUHUSU HOMA YA KIRUSI CHA KORONA
Homa ya kirusi cha korona ni nini?
Ni ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaombatana na mafua makali unaosababishwa na virusi vya corona ni ugonjwa unaoshambulia mfumo mzima wa hewa.
  • Ni aina ya maambukizi yanayoathiri mapafu kwa kawaida ugonjwa huu unaenezwa kwa kasi sana na kirusi kiitwacho ‘novel coronavirus’.
  • Virusi vya aina hii huwa kwa kawaida vinawaathiri wanyama lakini mara nyingine vinaweza kuwapata binadamu, kwa mfano mlipuko wa ugonjwa wa ‘Sars’ ambao uliuwa watu wengi China katika miaka ya nyuma.
  • Ugonjwa wa Sars ni ugonjwa hatari sana ambao nao huenezwa kwa mfumo wa hewa unaoenea kwa kasi mno.
Dalili za homa ya kirusi cha corona
  • Homa kali, 
  • Kukohoa
  • Kupumua kwa shida
  • Mwili kuchoka
  • Kuumwa kichwa
  • Maumivu ya misuli
  • Vidonda kooni



  • Aidha katika kipindi cha kupata maambukizi mpaka kuonekana kwa dalili za ugonjwa ni kati ya siku 2 hadi 10.

Jinsi ugonjwa wa corona unavyoambukizwa
Ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya hewa au kwa kugusa majimaji au kamasi kutoka kwa mtu mwenye virusi vya corona.

Jinsi ya kujikinga
  • Nawa mikono kwa maji safi yanayo tiririka na sabuni mara kwa mara
  • Funika mdomo na pua wakati wa kupiga chafya au kukohoa kwa kutumia kitambaa kisafi au sehemu ya mbele ya kiwiko cha mkono wako.
  • Epuka kumshika mkono mtu mwenye dalili za ugonjwa huu
  • Kaa mbali na mtu mwenye mafua au kikohozi ambaye ana historia ya kusafiri nje ya nchi.


  • NB:.Ugonjwa huu hutibiwa kufuatana na dalili zilizojitokeza, ambapo mpaka sasa hakuna chanjo maalumu kwa ajili ya ugonjwa huu.
  • Kwasasa wananchi tunaombwa kupunguza utamaduni wa kusalimiana kwa kupeana mikono na kukumbatiana.
                                    Hii ni njia njia mbadala ya kusalimiana iliyopendekezwa😊😊
MWISHO
Huu ndio mwisho wa elimu yetu hii ya leo iliyokuwa inahusu HOMA KALI YA MAPAFU INAYOSABABISHWA NA KIRUSI CHA CORONA tukutane kwenye masomo mengine.
ASANTENI.

Comments